Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 23, 2017

SERENGETI BOYS WAKATIWA BIMA ZA AFYA







WACHEZAJI wa timu ya Taifa ya soka ya Vijana waliochini ya miaka 17, ‘Serengeti boys’ wamekabidhiwa bima za Afya na Mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF)
Akizungumza wakati ya hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya NHIF, Kurasini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano,  Angela Mziray alisema afya ni mtaji wa kwanza kwa mtu hivyo wameamua kuwekeza kwa wachezaji wa Serengeti boys kwa vile wanaitangaza vema Tanzania.
“Serengeti boys wameitangaza vema Tanzania na sisi tukaona tutumie fursa hii kujitangaza kwa sababu wanatuwakilisha kimataifa hivyo tunawakabidhi Toto Afya kadi kila mmoja, “ alisema Angela.
Pia Angela alisema si mara yao ya kwanza kufanya kazi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwani tayari ni wadhamini wenza kwenye ligi kuu.
Naye Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa aliishukuru NHIF kwa kuwapatia bima wachezaji hao kwani TFF ilikuwa inatumia pesa nyingi kuwahudumia pindi wanapougua au kupata majeraha wakiwa kambini.
“Naipongeza NHIF kwa kuwapatia bima wachezaji wa Serengeti boys na nawapomba msiishie kwenye timu hii tu bali na timu nyingine za taifa na klabu,” alisema Mwesigwa.
Toto Afya kadi ni bima kwa watoto wenye umri wa kuanzia siku moja hadi miaka 18 na huchangiwa sh. 50,600 kwa mwaka.
NHIF imefika asilimia 90 nchi nzima wakiwa na vituo zaidi ya  6000 kwa ajili ya kutoa huduma ya bima ya afya.

No comments:

Post a Comment