WACHEZAJI timu ya soka ya Taifa ya Vijana waliochini ya miaka
17, 'Serengeti boys', wamefurahia kufuzu fainali za Vijana zitakazofanyika
Gabon kuanzia April, 2.
Wakizungumza na gazeti hili jana asubuhi
baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Yohana
Mkomola alisema amefurahi kusikia Tanzania imeshinda rufaa walioikatia Congo
Brazaville.
"Tuna uwezo wa kufanya vizuri hivyo
kushinda rufaa tunakwenda kuonesha Afrika kuwa hatukubahatisha kufuzu bali
uwezo tunao," alisema Mkomola.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya soka la
Vijana ya TFF, Ayoub Nyenzi aliwataka wachezaji hao kuwa watulivu wakati huu
bali waendelee na programu ya kocha kwa umakini.
"Kipindi hiki ni kigumu kwetu,
tunatakiwa kujiandaa kwa mashindano kwani fainali zinaanza Aprili 2, hivyo
umakini wetu uwe kwa makocha na kufuata kile kitakachoambiwa na makocha,"
alisema Nyenzi.
Tanzania imepangwa kundi B na timu za
Niger, Mali na Angola kwenye fainali hizo ambazo zitaanza April 2 nchini Gabon.
Tanzania iliondolewa kwenye mbio za kufuzu na
Congo Brazaville kwa faida ya bao la ugenini baada ya mchezo wa awali kushinda
3-2 nyumbani na ugenini kufungwa bao 1-0.
Tanzania kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliikatia rufaa
Congo Brazaville kwa kumchezesha
Langa-Lesse Bercy aliyekuwa amezidi umri na juzi kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) limeirejesha Tanzania kushiriki katika
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17
baada ya kushinda rufaa yake.
TFF ilikata rufaa kupinga kuchezeshwa
kwa mchezo huyo, ambapo Caf iliamuru afanyiwe vipimo vya kugundua umri wake
halisi, lakini mara mbili mchezaji huyo
hakutokea
No comments:
Post a Comment