Dar es salaam, 07/02/2017, uongozi wa taasisi ya tiba ya
mifupa muhimbili [MOI] unauarifu umma kwamba bwana mohamed rashid matumla (30)
alipokelewa katika chumba cha wagonjwa wa dharura MOI jana alfajiri tarehe
06/02/2017 Alipokelewa akiwa na maumivu makali ya kichwa na hali ya kupoteza
kumbukumbu na fahamu Alifanyiwa uchunguzi wa kina pamoja na kupata vipimo
mbalimbali ikiwemo vya CT-SCAN ya ubongo ambapo tulibaini kuwa amepata jeraha kichwani na kwenye ubongo ambalo limepelekea damu
kuvilia kwenye ubongo kitaalamu (Acute subdural hematoma) na kusababisha
Mgandamizo kwenye ubongo upande wa kulia ambapo alihitaji upasuaji wa haraka na
wa dharura, baada ya vipimo jana saa 3 asubuhi bwana mohamedi matumla
aliingizwa katika chumba cha upasuaji kwa ajili ya upasuaji mkubwa wa ubongo
(craniotomy)na kuondoa damu iliyo vilia kichwani. Aidha, tunapenda kuwaarifu
kwamba upasuaji huo ulifanyika kwa mafanikio makubwa na ulifanywa na jopo la
wataalamu wetu wazalendo 5 kwa muda wa masaa 3 Baada ya upasuaji huo
tumejiridhisha kwamba bw mohamed matumla yuko salama na ameondolewa kwenye
hatari ya kupoteza maisha, pamoja na mambo mengine, Taasisi ya MOI inapenda
kuwataarifu watanzania na wapenzi wa mchezo wa ndondi kwamba mohamed matumla
ataweza kurudi katika hali yake ya kawaida katika kipindi cha miezi 8 hadi 12
ambapo ataweza kucheza mchezo wa ngumi baada ya kupata kibali maalumu cha
daktari IMETOLEWA NA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI MOI DR,OTHMAN KILOLOMA 7TH
FEBRUARY 2017
No comments:
Post a Comment