Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 10, 2017

Shamrashamra za Burudani za Uzinduzi wa Tamasha la Sauti za Busara

Mwenyekiti wa Tamasha la Busara Zanzibar, Simai Mohammed Said akiwa na Mabalozi wa Norway na Uswisi kulia kwa Simai ni Balozi wa Uswisi Tanzania, Florence Tinguely na Balozi wa Norway Tanzania, Hanne Marie wakiangalia wakiangalia vikundi vya Utamaduni wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Sauti za Busara katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Kisongo wakiangalia burudani.
Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni kutoka Nchini Burundi wakitoa burudani katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Zanzibar kabla ya kuanza kwa maandamano ya Uzinduzi yalioanzia katika viwanja hivyo hadi katika viwanja vya bustani ya Forodhani.
Wasanii kutoka burundi wakionesha umahiri wao wa kupiga ngoma za utamaduni wa kwao. 


Wananchi waliofika katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani wakifuatilia burudani za wasanii mbalimbali kabla ya kuaza kwa maandamano ya ufunguzi wa Tamasha la Busara Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar akitowa maelezo kwa Mabalozi wa Uswisi na Norway walipokuwa katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu wakipata maelezo ya Mnara huo

Kikundi cha Six Unity wakionesha umahiri wao wa kujenza Dance wakati wa uzinduzi huo katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani.
Wasanii wakitoa burudani
Wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi Jangombe wakicheza ngoma ya Bomo


Wananchi wakifuatilia burudani zilikuwa zikitolewa  na Vikundi mbalimbali vya Utamaduni vinavyoshiriki Tamasha la Busara Zanzibar.
Imeandaliwa na OthmanMapara.
Zanzinews.com.
othmanmaulid@gmail.com.