Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 10, 2017

RATIBA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI HII, ARSENAL v HULL CITY MAN UNITED v WATFORD, LIVERPOOL vs TOTTENHAM HOTSPURS


Wikiendi hii EPL, Ligi Kuu England, itaanza kupigwa Jumamosi Mchana kwa Mechi ya awali huko Emirates kati ya Arsenal na Wababe wa Liverpool, Hull City.
Jumamosi iliyopita Hull City walileta msisimko mkubwa kwa kuitwanga Liverpool 2-0 na sasa Wadau macho kodo kuona kama wataweza pia kuwatenda Arsenal ambao nao walinyukwa 3-1 na Chelsea.
Baadae Siku hiyo Saa 12 Jioni, Saa za Bongo, zipo Mechi nyingine 5 na mojawapo ni ile ya huko Old Trafford kati ya Manchester United na Watford.
Ikiwa Man United watashinda Mechi hii basi watatoka Nafasi ya 6 walioshikilia kwa muda mrefu na kupanda hadi Nafasi ya 5 juu ya Liverpool na pengine kufika hadi Nafasi ya 4 ikiwa Arsenal atafungwa na Hull City katika Mechi yao ya mapema.
Lakini mafanikio hayo ya Man United yanaweza yakawa ni ya muda tu kwani baadae hiyo Jumamosi ipo Mechi moja ya mwisho ya EPL huko Anfield kati ya Liverpool na Tottenham.
Hiyo ni Mechi ngumu mno kwa Liverpool inayoshika Nafasi ya 5 na inayosuasua wakiwa hawajashinda hata Mechi 1 ya Ligi Mwaka huu 2017.
Spurs wao wako ngangali na ndio wanaoshika Nafasi ya Pili ya EPL wakiwa Pointi 9 nyuma ya Vinara Chelsea.
Jumapili zipo Mechi 2 ambapo Vinara Chelsea wako Ugenini kucheza na Burnley na pia Mabingwa Watetezi Leicester City wako Ugenini kuivaa Swansea City huku lengo lao kubwa likiwa si tena kuutetea Ubingwa wao bali kujinusuru kuporomoka Daraja kwani wanafanya vibaya na sasa wapo Nafasi ya 16 wakiwa Pointi 1 tu juu ya zile Timu 3 za mkiani ambazo hushushwa Daraja mwishoni mwa Msimu.
EPL itaendelea Jumatatu kwa Mechi 1 tu ambayo Man City wapo Ugenini kucheza na Bournemouth wakisaka ushindi ili kushika Nafasi ya Pili ikiwa Spurs atateleza kwa Liverpool.

RATIBA KAMILI
Jumamosi Februari 11

15:30 Arsenal v Hull City
18:00 Manchester United v Watford
18:00 Middlesbrough v Everton
18:00 Stoke City v Crystal Palace
18:00 Sunderland v Southampton
18:00 West Ham United v West Bromwich Albion
20:30 Liverpool v Tottenham Hotspur 


Jumapili Februari 12
16:00 Burnley v Chelsea
19:00 Swansea City v Leicester City
Jumatatu Februari 13
23:00 Bournemouth v Manchester City