MABONDIA
Meshack Mwankemwa wa Mbeya na Ramadhani Shauri kila mmoja ametamba kumpiga
mwenzake kwa KO kwenye pambano lao la raundi kumi, ubingwa wa Afrika Mashariki
na Kati utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakizungumza
na waandishi wa habari, Mwankemwa alisema hajaja Dar es Salaam kushangaa
ghorofa bali amekuja kuonesha namna ngumi zinavyopigwa.
"Sina
maneno kazi yangu ni ulingoni, naamini nitashinda kwa KO ya mapema ili
kudhihirisha ngumi zipo pia mikoani hasa Mbeya," alisema Mwankemwa.
Naye bondia
Shauri alisema jogoo wa shamba siku zote hawiki mjini maana hajui muda gani ni
asubuhi au ni usiku hivyo atampiga kipigo cha mwana ukome.
"Huku
mjini jogoo wa shamba hawiki hivyo kipigo nitakachompa hatakwenda kukihadithia
hata kwa watoto wake," alisema Shauri.
Promota wa
pambano huo Sadick Kinyogoli aliwataka mashabiki kufika kwa wingi kujionea
mpambano huo ambao utasindikizwa na mapambano mengine mengi ya kimataifa na ya
nyumbani.
"Mashabiki
wa ngumi waje kwa wingi kujionea mapambano haya kwani kuna mabondia wenye
vipaji," alisema Kinyogoli.
Mabondia
watakaosindikiza pambano hilo ni Mohamed Matumla ambaye atapambana na Mfaume
Mfaume, bondia Iddi Mkwela ataoneshana umwamba na Manyi Issa pambano la raundi
kumi zisizokuwa na ubingwa.
Pambano
lingine la ubingwa wa taifa utakuwa kati ya Said Chino na Twalib Tuwa ubingwa
wa taifa wa TPBC, mkanda ambao unatetewa na Tuwa.
Husein
Pendeza wa Ashanti Boxing clab ya Ilala atakaevaana na Said Hamdani kutoka
Mbezi Conetion na Mbwana
Matumla atazichapa na Suleimani Shabani
Pia
kutakuwepo na pambano la kimataifa wa kina dada
Anisha Bashir kutoka Malawi na Ester Boazi Kazeba wa Tanzania
No comments:
Post a Comment