Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 3, 2017

MWANKEMWA AWASILI DAR ES SALAAM KUPAMBANA RAMADHAN SHAURI JUMAPILI


Mabondia Meshack Mwankemwa wa Mbeya na Mbwana Matumla wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika Feb 5 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Mwankemwa atapanda ulingoni na Ramadhan Shauri.


Bondia Meshack Mwankemwa wa Mbeya ameingia Dar es salaam kwa ajili ya mpambano wake na Ramadhani Shauri mpambano utakaokuwa wa raundi kumi za ubingwa wa EAST/ CENTRAL AFRICA Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa Akizungumza na waandishi wa habari Promota wa mpambano huo Sadick Kinyogoli amesema kuwa huu ni wakati wa mwisho wa kuelekea mpambano utafanyika mwishoni mwa wiki hii
Aliongeza kwa kusema Mwankemwa ametuwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Shauri ndio kwao hivyo mpambano utakuwa mkali sana kwa kuwa mabondia wote wameshacheza mapambano makubwa ya kimataifa hivyo wapenzi waje kuangalia burudani ya masumbwi walioikosa kwa kipindi cha nyuma
Kinyogoli alisema kuwa bondia Mohamed Matumla atapambana na Mfaume Mfaume wakati bondia chipukizi Iddi Mkwela ataoneshana umwamba na Manyi Issa mpambano wa raundi kumi zisizokuwa na ubingwa
Mchezo mwingine wa ubingwa wa taifa utakuwa kati ya Said Chino na Twalib Tuwa ubingwa wa taifa wa TPBC mkanda ambao unatetewa na Tuwa  Husein Pendeza wa Ashanti Boxing club ya Ilala atavaana na Said Hamdani kutoka Mbezi Connetion na Mbwana Matumla atazichapa na Suleimani Shabani
Pamoja na mpambano mwingine wa kimataifa wa kina dada Anisha Bashir kutoka Malawi na Ester Boazi Kazeba wa Tanzania
Aliongeza kwa kusema kuwa mabondia wote watapima uzito pamoja na Afya zao kesho katika hotel ya Atrium iliyopo sinza Afrika sana