Kamati
ya Bodi ya Ligi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72),
imemfungia Kocha wa Stand United, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kushiriki michezo
mitatu uwanjani na faini ya Sh 500,000 (laki tano).
Katika mechi Na. 160 ya Ligi Kuu ya
Vodacom uliozikutanisha timu za JKT Ruvu na Stand United iliyochezwa Januari
30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Morocco aliondolewa
kwenye benchi (Ordered off) kwa kosa la kupiga maamuzi ya mwamuzi na kutoa
lugha chafu.
Kamati hiyo ya Saa 72 imechukua
hatua hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 40 (11) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa
Makocha. Morocco hata kama atakuwa amemaliza mechi tatu nje ya benchi,
hataruhusiwa kukaa kwenye benchi hadi awe amelipa faini hiyo.
Adhabu hiyo ya Morocco itaendelea
kumhusu hata kama utakuwa umehamia kwenye timu nyingine na katika msimu
mwingine wowote.
No comments:
Post a Comment