Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 1, 2017

MKWASA KATIBU MKUU YANGA Image result for MKWASA IMAGES
ALIYEKUWA kocha wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars', Charles Boniface Mkwasa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Yanga.
Mkwasa ambaye aliwahi kuwa mchezaji na kocha wa Yanga anachukua nafasi iliyokuwa inakaimiwa na Baraka Deusdedit anayerejea kwenye Idara ya Fedha.
Akizungumza na wandishi wa habari  jana Makao Makuu ya klabu hiyo Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema Mkwasa anaanza majukumu yake Februari mosi,  mwaka huu.
"Mkwasa ameteuliwa kushika wadhifa wa Katibu Mkuu nafasi ambayo ataanza kuitumikia Februari mosi, tunampongeza na tunamtakia kila la heri kwenye majukumu haya mapya," alisema Sanga
Akizungumza na gazeti hili, Mkwasa alishukuru uongozi wa Yanga kuona mchango wake na kumteuwa kwenye nafasi hiyo ya utawala.
"Nashukuru wameona mchango wangu kuanzia nikiwa mchezaji hadi kuwa kocha katika vipindi tofauti, nawaahidi utumishi uliotukuka, zaidi anaomba ushirikiano," alisema Mkwasa.
Mkwasa anarejea Yanga ikiwa ni mwezi mmoja umepita tangu aache kuwa kocha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, nafasi ambayo imechukuliwa  na kocha Salum Mayanga.
Mkwasa aliifundisha Taifa Stars kuanzia  Julai mwaka 2015 akirithi mikoba ya Mart Nooij na aliiongoza timu hiyo katika mechi 13, ikishinda mbili, kufungwa sita na sare tano.