MSHAMBULIAJI kinda wa Tanzania ambaye anacheza timu ya Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 17, 'Serengeti boys', Yohana Mkomola amefuzu majaribio kwenye klabu ya Etoile du Sahel
Akizungumza
na gazeti hili kwenye kambi ya Serengeti boys, Mkomola alisema alipata dili la
kwenda kuichezea klabu hiyo maarufu barani Afrika baada ya kumalizika kwa hatua
ya makundi ya mashindano ya Vijana Afrika.
“Habari
hizo ni kweli nilienda Etoile du Sahel kufanya majaribio katika timu yao ya
U-20 kwa wiki mbili lakini nilifanya kwa wiki moja na nusu tu nikapata majibu
kuwa nimefuzu," alisema Mkomola.
Mkomola ambaye awali alikuwa kwenye kikosi cha
pili cha Azam FC aliamua kuachana nao baada ya kuona hawamwitaji.
Kwa sasa Mkomola mwenye miaka 16 yupo kwenye
kambi ya Serengeti boys ambayo inajiandaa na fainali za Vijana za Afrika
zitakazofanyika April baada ya kushinda rufaa.
Tanzania iliondolewa kwenye mbio za kufuzu na
Congo Brazaville kwa faida ya bao la ugenini baada ya mchezo wa awali kushinda
3-2 nyumbani na ugenini kufungwa bao 1-0.
Tanzania kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliikatia rufaa
Congo Brazaville kwa kumchezesha
Langa-Lesse Bercy aliyekuwa amezidi umri na juzi kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) limeirejesha Tanzania kushiriki katika
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17
baada ya kushinda rufaa yake.
TFF ilikata rufaa kupiga kuchezeshwa
kwa mchezo huyo, ambapo Caf iliamuru afanyiwe vipimo vya kugundua umri wake
halisi, lakini mara kadhaa mchezaji huyo
hakutokea
No comments:
Post a Comment