Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, February 4, 2017

LIPULI YAWA TIMU YA KWANZA KUPANDA LIGI KUU MSIMU UJAO


TIMU ya Lipuli imekuwa timu ya kwanza toka daraja la kwanza kupanda Ligi Kuu msimu ujao baada ya jana kuifunga Polisi Dar es Salaam mabao 3-1 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.

Lipuli ambayo ilicheza mbele ya mashabiki wake imeandika historia hiyo kwani tangu 1996 ndio mara ya mwisho kwa mkoa wa Iringa kushiriki ligi kuu bila kufungwa nyumbani.

Kwa matokeo hayo Lipuli imefikisha pointi 29 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye kundi A huku ikiwa na michezo miwili mkononi, mmoja dhidi ya Ashanti United na mwingine dhidi ya Pamba.