Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 8, 2017

AZAM FC YALIA NA TFF KUHUSU RATIBA

UONGOZI wa Azam FC umesema mabadiliko ya ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara yanayofanywa na Shirikisho la mpira nchini (TFF) yanaharibu mipango ya kocha kufanya maandalizi ya michuano kombe la Shirikisho barani Afrika.Kauli hiyo imekuja baada ya kupokea barua pepe kutoka TFF ikiwataarifu kuwa mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting utachezwa Uwanja wa Mabitini, Februari 11 wakati walikuwa wakijipanga na mechi ya Mwadui FC ya Februari 19 hivyo imeharibu utaratibu wa kocha Aristica Cioaba.
Akizungumza na gazeti hili, Ofisa Habari wa klabu hiyo Jaffar Idd alisema mabadiliko ya mara kwa mara yanawaumiza kwakuwa yanaingilia programu za kocha na mchezo dhidi ya  Ruvu ulikuwa haujapangiwa tarehe lakini jana wamepokea barua hivyo hawana jinsi watabidi wacheze kwakuwa ndiyo inavyotakiwa.
“Tutacheza na Ruvu Februari 11, baadae tutacheza na Mwadui Februari 19 kabla ya kukutana na Mtibwa Sugar nyumbani Februari 24 kabla ya kombe la Shirikisho ndipo tutaanza maandalizi ya mechi za kimataifa,” alisema Jaffar.
Katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Azam itaanzia nyumbani kwa kucheza na mshindi kati ya timu za Opara United ya Botswana na Mbabane Swallow ya Switzerland mchezo utakaochezwa Machi 10 na 12.
Jaffar alisema pia watatumia mechi za ligi kujipima kabla ya kucheza mechi ya kombe la Shirikisho kwakuwa muda uliobaki ni mdogo na hawataweza kupata mechi ya kirafiki kutoka nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment