Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 27, 2017

SIMBA NA AZAM FC RUKSA UWANJA WA TAIFA KESHO





Na Rahel Pallangyo
SIMBA na Azam FC zitashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu baada ya serikali kufungulia uwanja huo ambao ulifungwa kutokana na mashabiki wa Simba kung'oa viti wakati wa mchezo wa raundi ya kwanza dhidi yao na Yanga.
Katika taarifa ya serikali ambayo ilitumwa kwenye vyombo vya habari na kusainiwa na Kaimu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Zawadi Msalla inasema Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnaye ameridhishwa na ukarabati wa miundo mbinu ya uwanja huo baada ya kuharibiwa Octoba Mosi, 2016.
"Nape amewataarisha wapenzi wa michezo kutunza mali za serikali kwa manufaa ya watanzania wote na kwa kushirikiana na vyombo vya usalama watawachukuliwa hatua mtu mmoja mmoja kwani kamera zilizofungwa zitasaidia kuwabaini kila atakayefanya tukio la uhalifu," alisema Zawadi.
Naye Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Alfred Lucas, alitoa shukrani kwa Waziri Nape kwa niaba ya wadau na mashabiki wa soka Tanzania na kuwataka kuwa wastarabu wanapokuwa ndani ya uwanja huo.
"Tunawaomba watanzania na mashabiki wa soka kuwa na nidhamu na kushangilia kistaarabu kwani uwanja mzima umefungwa kamera ambazo zina uwezo wa kuwatambua kila mmoja," alisema Lucas
Kwa upande wa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Simba, Haji Manara alisema kufunguliwa kwa uwanja ni surprise kwao na kuwataka mashabiki wao kuwa na uvumilivu pindi timu inapopata matokeo ambayo hayaridhishi.
"Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushangilia timu yao lakini pia wanatakiwa kuwa na uvumilivu japo matokeo mengine yanasababishwa na maamuzi mabaya ya marefa wetu, TFF mlifanyie kazi," alisema Haji.
Pia Haji alisema timu ikifungwa kihalali hakuna mtu anayelalamika na kudai aliposema mchezo dhidi ya mahasimu wao Yanga uchezeshwe na waamuzi toka nje ya nchi alijua fika kanuni haziruhusu bali alifanya hivyo ili wabadilike.
Uwanja wa Taifa ulifungwa na Waziri Nape kufuatia uharibifu uliofanyika Oktoba Mosi, 2016 kwenye mchezo wa Simba na Yanga mashabiki wa Simba wakipinga bao lililofungwa na Amis Tambwe kwa madai kabla ya kufunga alikuwa ameshika mpira
Mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Martin Saanya ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1, bao la Simba likifungwa na Shiza Kichuya kwa mpira wa kona.

No comments:

Post a Comment