Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 13, 2017

Pogba kukabidhiwa unahodha Man United

Maisha ya nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney ndani ya kikosi cha timu hiyo yanaonekana kwenda ukingoni kutokana na umri wake lakini ikiwa bado haijajulikana ni nani ambaye atachukua kitambaa cha unahodha baada ya yeye kuondoka.
Kocha wa Man United, Jose Mourinho amemtaja mchezaji ambaye anaweza kuchukua nafasi ya Rooney ni Paul Pogba ambaye wamemsajili kutoka Juventus, kwani mchezaji huyo raia wa Ufaransa ana uwezo wa kucheza soka ambalo linawavutia watu wengi na anaamini anaweza kuwa kiongozi mzuri kwa wachezaji wenzake.
“Nafikiri anaweza. Nafikiri ana uwezo mkubwa, anacheza kwa malengo, anaelewa nini anafanya. Ni mchezaji bora, licha ya umri wake kuwa mdogo lakini tayari ana vitu vingi, nadhani anaweza,” alisema Mourinho.
Kuhusu mchezo wa kesho Jumapili dhidi ya Liverpool na jinsi ambayo Man United itacheza kumzunguka Pogba, Mourinho alisema, “Sio sawa kusema mchezaji anapaswa kuwa bora, anacheza vizuri, ndiyo, hakuna shaka kuhusu hilo, lakini timu inacheza vizuri, sitegemei kama timu inaweza kucheza vibaya na kumbebesha mzigo mchezaji mmoja. Sio Paul au yoyote, nategemea timu itacheza vizuri na Paul kucheza katika kiwango chake.”