Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 24, 2017

LIGI YA WANAWAKE KUENDELEA KESHOLIGI Kuu ya wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo sita kuchezwa kwenye makundi yote.
Kundi A, linatarajiwa kuna na mchezo kati ya JKT Queens na Mburahati Queens za Dar es Salaam utakaofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala.
Kadhalika Viva Queens ya Mtwara itakuwa mwenyeji wa Evergreen ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara wakati Mlandizi ya mkoani Pwani itakuwa mgeni wa Fair Play katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Kwa upande Kundi B, Sisterz ya Kigoma itaikaribisha Baobab ya Dodoma kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma.
Mchezo mwingine utachezwa Uwanja wa Samora mkoani Iringa kati ya Panama na Majengo Women ya Singida ilihali Victoria Queens ya Kagera na Marsh Academy zitapambana kwenye Uwanja wa Kaitaba Kagera.