Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 18, 2016

WASANII WA TANZANIA WAULA






SERIKALI ya Tanzania na Afrika Kusini zimekubaliana kushirikiana katika nyanja ya filamu, haki za ubunifu pamoja na kuandika historia ya ukombozi kusini mwa bara la Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema yeye pamoja na Waziri wa Utamaduni wa Afrika Kusini, Nathi Mthethwa wamekubaliana kushirikiana kwenye eneo la sanaa.
Afrika Kusini wameendelea kwa upande wa sanaa ndio maana unaona wasanii wengi hapa nchini wanakwenda kutengeneza filamu huko hivyo tumekubaliana kushirikiana kwani sheria wamefanikiwa kutengeneza mifumo ya kisheria ya kulinda haki za wasanii na ubunifu, alisema Nape.
Pia Nape alisema Serikali ya Tanzania pamoja na Afrika Kusini mwaka 2011  waliingia makubaliano ya kushirikiana, jambo ambalo lilifuta viza na kukubaliana kuandaa historia ya kupigania uhuru kwa nchi za kusini mwa bara la Afrika.
Nape alisema makubaliano hayo yataleta mabadiliko katika sanaa kwa nchi yetu na kuongeza mahusiano ya nchi mbili kwa watu kwa watu na siyo nchi kwa nchi.
Moja ya makubaliano hayo ni kutengenezwa route of indepence kwa sababu isipoandikwa na nchi husika wengine wanaweza wasiiandike vizuri au wakaikosea na kwa mwaka huu wa fedha imetengewa Sh mil 700.
Waziri Nathi yupo nchini na ujumbe wa watu saba na jana wamekwenda Morogoro kutembelea makaburi ya Mazimbu na Dakawa na watakwenda Bagamoyo pamoja na Dar es Salaam, ambapo watatembelea jengo ambalo lilikuwa likitumika kwa vikao vya kupigania uhuru lililopo  pembeni ya jengo la ubalozi wa Msumbiji.
Mwanzo jengo hilo lilikuwa linatunzwa na jeshi lakini kwa sasa lipo chini ya Wizara ya Habari na lipo kwenye mpango wa kukarabatiwa.

No comments:

Post a Comment