Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 18, 2016

KIINGILIO BURE FAINALI ZA UCHEKESHAJI TABATA KESHOFAINALI ya msimu wa pili wa shindano la kusaka vipaji vya sanaa ya ucheshi linatarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa 40/40 Tabata, Dar es Salaam.
Jumla ya washiriki 18 waliopatika na kutoka wilaya za mkoa wa Dar es Salaam watapanda jukwaani kuonesha vipaji vyao na fainali hizo ni bure.
Akizungumza na gazeti hili Meneja wa Vuvuzela Company Ltd, Evans Bukuku alisema shindano hili litaendelea, kwani sanaa ya ucheshi inaweza kutengeneza nafasi kubwa kwa Watanzania wengi.
“Mshindi atapata pesa taslimu 2,000,000/= na mafunzo ya vitendo ya miezi 6
Mashindano haya yalianza Septemba 6, 2016 yakijumuisha zoezi la kusajili washiriki na fainali hizo zitasindikizwa na burudani kutoka Twanga Pepeta Band na kiingilio ni bure kwa watu waliotimiza miaka 18 na kuendelea.