Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, July 17, 2016

YANGA YABANWA NYUMBANI, KUENDELEA KUSHIKA MKIA







JUHUDI za Yanga kupata ushindi wa kwanza na kufufua matumaini ya kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC) hazijazaa matunda, baada ya jana kutoka sare ya bao 1-1 na Medeama ya Ghana, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo ya mchezo huo, Yanga inaendelea kushika mkia ikiwa na pointi moja katika kundi lake baada ya kumaliza duru la kwanza la michuano hiyo kwa kucheza michezo mitatu, wakati Medeama imefikisha pointi mbili na inashika nafasi ya pili kutoka mkiani.
Yanga ilianza michuano hiyo kwa kufungwa bao 1-0 na Mouloudia Olympique Bejaia (MO Bejaia) nchini Algeria kabla ya kufungwa 1-0 na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) mjini Dar es Salaam.
TP Mazembe inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi sita baada ya kushinda michezo yake miwili iliyopita dhidi ya Medeama na Yanga, wakati MO Bejaia inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi nne.
MO Bejaia iliifunga Yanga bao 1-0 na kutoka sare na Medeama, ambapo leo itaikaribisha TP Mazembe katika kukamilisha duru la pili la michuano hiyo.
Yanga bado ina nafasi ya kufanya vizuri  katika michuano hiyo, lakini itabidi ihakikishe haipotezi mechi zake tatu zilizobaki za duru la pili.
Duru la pili linatarajiwa kuanza Julai 26, ambapo Yanga itakuwa ugenini nchini Ghana kurudiana na Medeana, wakati TP Mazembe itaikaribisha MO Bejaia.
Kihesabu, Yanga itabidi iombe TP Mazembe ishinde leo, kisha yenyewe mchezo ujao nayo ishinde ifikishe pointi nne sawa na MO Bejaia, huku pia ikiomba Mazembe iifunge tena MO Bejaia zitakaporudiana.
Kama matokeo yakiwa hivyo ina maana tayari TP Mazembe itakuwa imekamata nafasi ya kwanza, ambapo Yanga, MO Bejaia na Medeama zitakuwa zinawania nafasi ya pili.
Katika mchezo wa jana, Yanga ilipata bao dakika ya kwanza tu mfungaji akiwa Donald Ngoma baada ya Simon Msuva kuingia katika eneo la hatari na kutoa pasi kwa mfungaji.
Kuingia kwa bao hilo kuliwapa imani mashabiki wa Yanga kwamba huenda timu yao ingeibuka na ushindi mnono zaidi hasa kutokana na Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm kuwahi kuinoa Medeama hivyo kuifahamu vizuri, lakini wageni walitulia na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.
Medeama ilisawazisha dakika ya 17, mfungaji akiwa Benard Danso akiunganisha mpira wa kona huku beki Vicent Bossou na kipa Deogratius Munishi wakibaki wameduwaa.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza timu hizo zilishambuliana kwa zamu huku wageni wakifanya mashambulizi ya kushtukiza zaidi, wakati Yanga ikipoteza nafasi nyingi za kufunga.
Yanga itabidi ijilaumu kutokana na kushindwa kutumia nafasi kadhaa ilizopata kipindi cha pili ama kwa kushindwa kulenga lango au kupiga mipira iliyookolewa na kipa wa Medeama.
Moja ya nafasi hizo ni ile ya dakika ya 70, ambapo shuti la kiungo Thabani Kamusoko liliokolewa na kipa, ambapo dakika tatu baadaye Ngoma alishindwa kufunga kwa kichwa.
Nafasi nyingine nzuri kwa Yanga ilikuwa dakika ya 59 wakati Juma Abdul alipoingia katika eneo la Waghana na kupiga krosi kwa Ngoma, lakini tiktak aliyopiga mshambuliaji huyo iliokolewa na kipa wa Medeama.
Yanga: Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Juma Mahadhi, Kelvin Yondani, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Obrey Chirwa, Amissi Tambwe/Haruna Niyonzima na Ngoma.

No comments:

Post a Comment