Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, July 26, 2016

WAAMUZI WATANO WENYE BEJI ZA FIFA WAFELI MTIHANI WA FITNESS


WAAMUZI watano wenye beji za FIFA wa Tanzania wamefeli mtihani wa utimamu ulifanyika juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mtihani huo ambao ni maalumu kwa ajili ya msimu mpya wa kupewa beji mpya na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulianza juzi na unatarajiwa kumalizika kesho.
Waamuzi waliofeli ni John Kanyenye, Waziri Sheha, Kudra Omar, Grace Wamara huku Sophia Mtongori yeye hakufika kwenye mtihani huo.
Kozi hii ambayo inaendeshwa na wakufunzi wa kimataifa Carlos Henrique, Mark Mzengo na Felix  Tangawarima ilikuwa na waamuzi 30 huku 18 ni wale wenye beji na 12 ni watarajiwa (elite)
Waamuzi hao waliripoti Julai 24 na juzi waliingia kwenye mtihani wa utimamu mwili na kuanzia jana wanaendelea na kudurusu marekebisho ya sheria 17 za soka ambalo zimefanyiwa marekebisho.

Gazeti hili lilishuhudia waamuzi hao wakitafsiri kwa vitendo sheria huku wakisimamiwa na wakufunzi wao.

No comments:

Post a Comment