Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, July 26, 2016

SERIKALI YAVIONYA VYAMA VYA MICHEZO NA KLABU

SERIKALI imevitaka Vyama, Mashirikisho na klabu za Michezo nchini kufuata taratibu na sheria zinazoendesha michezo na kuacha kutumia vyombo vya habari kama mawakala.
 Akizungumza na wandishi wa Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja, alisema vyombo vyote vilivyo chini ya ofizi yake vinafahamu hatua mbalimbali za kupitia katika kutatua  tatizo au changamoto kwakuwa zinaongozwa na katiba
“Naviagiza Vyama, mashirikisho na klabu kufuata taratibu na sheria zinazowaongoza katika kuendesha michezo na kutatua matatizo yao na kwa kuzingatia miongozo ili kuleta maendeleo ya michezo nchini badala ya kuwatumia Wanahabari katika kutafuta ufumbuzi wa mambo yao” alisisitiza Kiganja.
Pia Kiganja alisema hasara za kutumia vyombo vya habari kunadi migogoro kunasababisha wadhamini kukata tamaa kusaidia sekta ya michezo na kuongeza kuwa serikali badala ya kushughulikia maendeleo ya michezo, inageuka mahakama au wasikiliza migogoro kwani mwenendo wa michezo inapata taswira mbovu kwa ajili ya watu wachache wenye uroho na tamaa za madaraka
Kiganja alisema baraza linavitaka vyama vya michezo nchini kujifanyia tathmini kama usajili wao unafanana na kazi wanazoziratibu kulingana na matakwa ya usajili wao.
Kiganja alieleza kuwa, serikali imeajiri maafisa mchezo mikoa yote, hivyo wawasiliane nao ili vyama hivi vishuke huko Mikoani, Wilayani hadi kwenye kata ambako ndiko wanamichezo wengi walipo na kuache kung’ang’ania kukaa na kufanya kazi Dar es salaam.

 “Miaka ya 1980-90 Tanzania ilikuwa inaongoza katika michezo mingi ndani ya Afrika Mashariki, lakini leo hii tunanunua wachezaji kutoka Burundi, Rwanda, Kenya, na Uganda, hivi tatizo letu Tanzania ni nini” ? aliuliza Kiganja.