Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 20, 2016

NAMUNGO YAPIGWA FAINI YA 500,000 KILA MCHEZO LAKINI YAPANDISHWA DARAJA

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeipiga faini ya Sh. 500,000, Klabu ya Namungo FC ya Lindi kwa kila mechi ambayo mchezaji Imani Vamwanga aliichezea timu hiyo akitumia jina la Emmanuel T. Mwanga katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL), kituo cha Morogoro 2015/2016.

Katika kikao kilichoketi Julai 14, 2016 kujadilina, kupitia, malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za mashindano ya RCL katika kituo cha Morogoro, kamati imebaini kwamba Namungo ilifanya udanganyifu wa jina la mchezaji kwa kumsajili na kumchezesha mchezaji Imani Vamwanga leseni Na. 930909003 ya usajili wa Ligi Daraja la Kwanza FDL msimu wa 2015/2016 klabu ya Kurugenzi Mafinga akitumia jina la Emmanuel T. Mwanga.

Kamati imebaini hayo kupitia taarifa za usajili, ripoti za waamuzi na makamisaa kwa michezo ambayo mchezaji tajwa hapo juu amecheza katika Mashindano ya Ligi ya mkoa wa Lindi na Mashindano ya Ligi ya Daraja la Kwanza FDL msimu wa 2015/16. Namungo inaadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 39 (1) inayozungumza adhabu kwa klabu.

Kamati ya Mashindano ya TFF imetoa uamuzi huo kwa Namungo FC kupigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kila mechi ambayo mchezaji Imani Vamwanga akitumia jina la Emmanuel T. Mwanga amecheza katika mashindano ya RCL.

Pamoja na faini hiyo kwa kila mchezo ambao Namungo ilimchezesha mcheza huyo, timu hiyo Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeitangaza Namungo FC kupanda daraja kwenda Ligi Daraja la pili msimu wa 2016/2017 kama ilivyoainishwa kwenye kanuni ya 5 kipengere cha (4).

Kamati imejiridhisha kwa kupitia taarifa za usajili, ripoti za waamuzi na makamisaa kwa michezo ambayo ilikuwa inalalamikiwa imefikia uamuzi huo kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo. Kamati imeipongeza na kukutakia kila la heri katika michezo.
****
Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kutoa pongezi zake za dhati kwa Klabu ya Pepsi FC ya Arusha kwa kupata nafasi ya kupanda daraja na kuingia Daraja la Pili SDL msimu wa 2016/2017.

Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 5 kipengere cha (5) ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa RCL msimu wa 2015/2016.
Timu imefanikiwa kupata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya mabingwa wa Mikoa 2015/2016 kituo cha Singida na kuongoza kati ya timu zilizoshika nafasi ya pili katika vituo vilivyosalia ambavyo ni Njombe, Morogoro na Muleba. TFF inaItakia kila la kheri katika maandalizi ya kushiriki Daraja la Pili msimu wa 2016/2017.
****
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imewafungia wachezaji watatu, walioshiriki katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL), kituo cha Morogoro 2015/2016.

Kikao cha Kamati ya   TFF kilichokaa Julai 14, 2016 kujadilina kupitia malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa RCL kituo cha Mororgoro, kimebaini kwamba wachezaji Imani T. Mwanga, Fred John Lazaro na Brown Chalamila walifanya udanganyifu wa majina ili kukamilisha zoezi la usajili.


KUHUSU MCHEZAJI IMANI T. MWANGA

Kamati imepitia taarifa za waamuzi na Kamisaa pamoja na uthibitisho uliopatikana imemkuta na tuhuma za udanganyifu wa jina. Alitumia majina mawili tofauti. Imani Vamwanga ligi daraja la kwanza klabu cha Kurugenzi FC na Emmanuel T. Mwanga klabu cha Stand Misuna.

Kwa mujibu wa kanuni za ligi ya mabingwa wa Mikoa, kanuni ya 39 (1) Kamati imekufungia kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miezi 12. Adhabu hii inaanza toka tarehe ya kuandi kwa barua yake.

KUHUSU FRED JOHN LAZARO

Kikao cha Kamati ya Mashindano ya TFF kilichokaa Julai 14, 2016 kujadili na kupitia malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa RCL kituo cha Mororgoro, kimebaini kwamba Fred John Lazaro pamoja na klabu ya Stand Misuna FC walifanya udanganyifu wa majina ili kukamilisha zoezi la usajili.

Kupitia taarifa za waamuzi na Kamisaa pamoja na uthibitisho uliopatikana, imebainika Fred John Lazaro alifanya udanganyifu wa majina hivyo kuchezea klabu mbili tofauti katika msimu mmoja isivyo halali.

Katika klabu ya Stand Misuna FC iliyoshiriki ligi ya mkoa Singida na ligi ya mabingwa wa mikoa kituo cha Morogoro 2015/2016 ulisajiliwa kwa jina la Fred John Lazaro kwa usajili namba 044 ukivaa jezi namba 13, pia katika klabu ya Singida United FC ya Singida iliyoko daraja la pili (SDL) msimu wa 2015/2016 ulisajiliwa kwa jina la Adolf Anthon leseni namba 950725003 ukivaa jezi namba 3, 6 na 8 katika mechi tofauti.

Kwa taarifa hapo juu kamati imebaini kuwa wewe siyo mchezaji halali kuichezea timu ya Stand Misuna FC katika ligi ya mabingwa wa mikoa kwa ni hukucheza ligi ya mkoa Singida, na pia kwa kushirikiana na uongozi wa klabu ya Stand Misuna FC umedanganya majina ili kufanikisha zoezi la usajili kinyume cha kanuni ya 48 kipengere cha (2) na (4).

Hivyo kwa mujibu wa kanuni za ligi ya mabingwa wa Mikoa, kanuniya 31 kipengere cha (11) na kanuni ya 39 kipengere cha (1) wewe Fred John Lazaro jezi namba 13 (mchezaji) unafungiwa kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miezi kumi na mawili (12).

Adhabu hiyo inaanza mara moja baada ya muhusika kupata barua yake.

KUHUSU BROWN CHALAMILA

Kikao cha Kamati ya Mashindano ya TFF kilichokaa Julai 14, 2016 kujadilina kupitia malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa RCL kituo cha Mororgoro, kimebaini kwamba Brown Chalamila pamoja na klabu ya Stand Misuna FC walifanya udanganyifu wa majina ili kukamilisha zoezi la usajili.

Kupitia taarifa za waamuzi na Kamisaa pamoja na uthibitisho uliopatikana umekutwa na makosa ya udanganyifu wa majina hivyo kuchezea vilabu viwili tofauti katika msimu mmoja isivyo halali.

Katika klabu ya Stand Misuna FC iliyoshiriki ligi ya mkoa Singida na ligi ya mabingwa wa mikoa kituo cha Morogoro 2015/2016 ulisajiliwa na kucheza kwa jina la Costa Bryan Bosco kwa usajili namba 029 ukivaa jezi namba 03, wakati wewe ni mchezaji halali wa klabu ya Kurugenzi FC ya Mafinga-Iringa iliyoko daraja la kwanza (FDL) msimuwa 2015/2016 leseni namba 921004001 ukivaa jezi namba 03.

Kwa taarifa hapo juu kamatii mebaini kuwa wewe siyo mchezaji halali wa timu ya Stand Misuna FC katika ligi ya mabingwa wa mikoa kwani hukucheza ligi ya mkoa Singida, na pia kwa kushirikia na uongozi wa klabu ya Stand Misuna FC ulidanganya majina ili kufanikisha zoezi la usajili kinyume na kanuni ya 48 kipengele cha (2) na (4) ya ligi ya mabingwa wa mikoa.

Hivyo, kwa mujibu wa kanuni za ligi ya mabingwa wa Mikoa, kanuniya 31 kipengele cha (11) na kanuni ya 39 kipengele cha (1) wewe Brown Chalamila unafungi wa kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miezi kumi na mawili (12). Adhabu hiyo inaanza mara moja kuanzia tarehe ya barua yakei.
****

Klabu ya Stand Misuna imepoteza ushindi kwa mechi zote ambazo imemchezesha mchezaji Brown Chalamila kwa jina la Costa Bryan Bosco, kwa mujibu wa Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kadhalika kamati hiyo imepigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kila mechi ambayo wachezaji Brown Chalamila akitumia jina la Costa Bryan Bosco na Adolf Anthon akitumia jina la Fred John Lazaro wamecheza katika mashindano ya ligi ya mabingwa wa mkoa RCL kituo cha Morogoro 2015/2016 

Pia, kamati hiyo imeamua kwamba Seif Juma Maulid ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Stand Misuna FC kupelekwa Kamati ya Nidhamu kwa tuhuma za kughushi na kukamilisha zoezi la usajili kwa udanganyifu.

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefikia uamuzi huo kwa mujibu wa Kanuni ya 53, na kanuni ya 48 (3), 48 (4), 9(21), 36 (6) na kanuni ya 39 (1) adhabu kwa klabu katika kikao kilichoketi Julai 14, 2016 kujadilina, kupitia, malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za mashindano ya RCL, Kituo cha Morogoro.

Kupitia malalamiko na vielelezo mbalimbali Kamati imebaini kwamba Misuna iliwasajili na kuwachezesha wachezaji Brown Chalamila akitumiaji na la Costa Bryan Bosco (3) na Adolf Anthony akitumia jina la Fred John Lazaro (13).



Wachezaji Brown Chalamila leseni namba 921004001 ni mchezaji halali wa klabu ya Kurugenzi FC ya Mafinga-Iringa na ameichezea Kurugenzi FC ligi ya daraja la kwanza FDL msimuwa 2015/2016.  Mchezaji Adolf Anthon leseni namba 950725003 ni mchezaji halali wa klabu ya Singida United na ameichezea Singida United ligi daraja la pili SDL msimu wa 2015/2016.

Kamati imebaini hayo kupitia taarifa za usajili, waamuzi na makamisaa kwa michezo ambayo wachezaji tajwa hapo juu wamecheza katika Mashindano ya Ligi ya mkoa wa Singida na Mashindano ya Ligi ya Daraja la Kwanza FDL na Daraja la Pili SDL ya TFF msimu wa 2015/16.

Katika mchezo namba 42B wa Ligi Daraja la Kwanza kati ya Kurugenzi FC na Lipuli FC uliochezwa tarehe 16/01/2016 uwanja wa Wambi Mafinga taarifa za kamisaa na mwamuzi zimeonesha mchezaji Brown Chalamila (3) alicheza mchezo huo, lakini pia tarehe hiyo hiyo katika mechi namba 3 ya Ligi ya mkoa wa Singida kupitia taarifa za kamisaa na mwamuzi inaonesha kwamba mchezaji Costa Bryan Bosco (3) usajili namba 029 amecheza katika kiwanja cha Namfua Singida katika mechi kati ya Stand MisunaFC naRuvu Sports Club.

Kamati imejiridhisha bila ya shaka yoyote kuwa mchezaji Brown Chalamila alicheza ligi ya mabingwa wa mikoa RCL 2015/16 kituo cha Morogoro, lakini hawakucheza katika mashindano ya ligi ya mkoawa Singida 2015/2016 na hivyo kupoteza uhalali wa usajili wake kwa muji
bu wa kanuni za mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa.

No comments:

Post a Comment