Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 23, 2016

MAN UNITED KUMSAINI POGBA, JOSE ADOKEZA KUWAGUSA ROONEY NA MATA.

Jose Mourinho ametoa ishara kubwa kwamba zile tetesi za Timu yake Manchester United kumsaini tena Kiungo wa France Paul Pogba kutoka Juventus zina ukweli aliposema: "Kukiwa na moshi, kuna moto!"
Zipo ripoti kuwa Man United wameshaafikiana na Juve kulipa Dau la Rekodi ya Dunia la Pauni Milioni 100 kumnunua Pogba, mwenye Miaka 23, alieondoka Man United kwenda Juve Mwaka 2012 bila Ada yeyote ile zaidi ya kulipwa Fidia ya kukuza kipaji ya Pauni 800,000 tu.

Mourinho pia amesema: "Nitakuwa mpuuzi kama pia sitasema tunajaribu kwa zaidi ya Mchezaji mmoja!"

Katika Kipindi hiki, Mourinho ameshasaini Wachezaji Watatu Wapya ambao ni Eric Bailly kutoka Villarreal, Henrikh Mkhitaryan wa Borussia Dortmund na Zlatan Ibrahimovic.

Alipoulizwa kuhusu kumsaini Pogba, Mourinho alijibu: "Tulilenga Mtu 4 na tumepata watatu na tutampata wa nne. Tuliamua Wanne ili kuboresha Kikosi kitupe uwezo wa kuwa na aina nyingi tofauti, kicheze kama ninavyolifikiria Soka."

Aliongeza: "Kila Mtu anamfikiria mmoja lakini haitanishangaza kama sio yeye na ni mwingine!"

Kuhusu Wayne Rooney, ambae amebakiza Bao 4 tu kuikamata Rekodi ya Sir Bobby Charlton aliefunga Bao 249 ambazo ni nyingi katika Historia ya Man United, Mourinho ameeleza: "Nashangaa kuhusu maswali mengi kuhusu huyu jamaa. Yeye ni Kepteni wa Klabu, ni Kepteni wa Meneja, ni Kepteni wa Wachezaji. Namwamini sana. Nadhani atakuwa Mchezaji muhimu kwangu!"

Mara mbili akiwa na Chelsea Mourinho alitoa Ofa za kumnunua Rooney na zote kukataliwa na Man United.

Kuhusu Juan Mata ambae aliuzwa na Chelsea kwenda Man United Mwaka 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 37.1, Mourinho amesema ipo nafasi kwa Mata kubaki kwenye Timu na kupigania nafasi.

Mourinho alifunguka: "Kwanza bora niweke mambo sawa kuhusu Klabu yetu iliyopita kwa sababu sikwambia Mata aondoke. Sikulazimisha auzwe. Ulikuwa uamuzi wake binafsi kuhama na mimi sipendi Wachezaji kuondoka. Kama Mchezaji hataki kubaki nasi basi kwa heri. Lakini nadhani sasa ana furaha na sidhani kama ataomba kuondoka."