Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 23, 2016

CAF YAPATA MDHAMINI MPYASHIRIKISHO la Soka barani Africa (CAF) limepata mdhamini mpya baada ya kumalizika kwa mkataba wake na kampuni ya mawasiliano ya Orange.
Orange imekuwa mdhamini mkuu wa mashindano makubwa ya CAF kwa miaka minane tangu 2009.
Kabla ya hapo, kampuni nyingine ya mawasiliano ya MTN ndiyo iliyokuwa mdhamini kwa miaka minne.

Sasa, mdhamini mpya atakuwa kampuni ya mafuta na gesi ya Total kutoka Ufaransa.
Kampuni hiyo itaanza kwa kudhamini michuano ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwaka 2017 ambayo itaandaliwa nchini Gabon. Thamani ya mkataba huo haijafichuliwa.

Total itakuwa mdhamini mkuu wa:

Kombe la Taifa Bingwa Afrika

Ligi ya Klabu Bingwa Afrika

Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN)

Super Cup ya Afrika

Kombe la Mashirikisho

Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa Wanawake

Kombe la Futsal Afrika

Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 23

Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 20

Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 17.