Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 20, 2016

ARSENE WENGER KUENDELEA KUWEPO EMIRATES HADI 2017

WACHAMBUZI huko England wamechokonoa kuwa n’ngwe ya mwisho ya Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ndio inaanza sasa kwa Mkongwe huyo ambae hajatwaa Taji la Ubingwa wa England tangu 2004.
Wachokonoaji hao wanaamini kuwa Wenger atafikia hatima ya himaya yake huko Emirates ikiwa Msimu huu mpya Arsenal haitatwaa Ubingwa huku yeye akiwa amebakiza Mwaka Mmoja tu katika Mkataba wake na Arsenl unaomalizika Mwakani 2017.
Kwa sasa, huu ndio Msimu wa mwisho kwa Wenger na ikiwa hatatwaa Ubingwa, bila shaka, shoka litamkuta.
Baada ya kumsaini Kiungo wa Uswisi Granit Xhaka katika kipindi hiki, Wachambuzi wanahisi Wenger anapaswa kuimarisha safu yake ya mashambulizi hasa baada ya Straika wake mkuu Olivier Giroud kuonyesha wazi hana uwezo wa kuibeba Arsenal kutwaa Ubingwa.
Straika wao mwingine, Danny Welbeck, yuko nje kitambo akiuguza Goti lake na Wenger alijaribu kumnunua Straika wa Mabingwa wa England Leicester City Jamie Vardy Straika huyo akaigomea Arsenal na kuamua kubaki Leicester.


Pia zimekuwepo ripoti kuwa Wenger anamuwania Straika wa Argentina Gonzalo Higuain anaechezea Napoli ya Italy lakini Dau lake la Euro Milioni 94 lipo nje ya uwezo wa kawaida wa Wenger alivyozoea kununua Wachezaji Bei chee.
Arsenal wanaanza matayarisho ya Msimu mpya kwa kusafiri kwenda Marekani kucheza na Kombaini ya Mastaa wa USA, MLS All-Stars, wanaocheza Ligi ya Marekani MLS. 

ARSENAL 2016-17 PRE-SEASON FIXTURES
Alhamisi Julai 28, 0300: vs MLS All-Stars (Avaya Stadium, San Jose)
Jumapili Julai 31, 1900: vs Chivas de Guadalajara (Stub Hub Centre, California) Ijumaa Agosti 5, 2130: vs Viking FK (Viking Stadion, Norway)
Jumapili Agosti 7, 2000: vs Manchester City (Ullevi Stadium, Sweden – International Champions Cup)