Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, June 17, 2016

WAPYA YANGA RUKSA KUKIPIGA KOMBE LA SHIRIKISHOSHIRIKISHO la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) limetuma leseni za wachezaji wanne wapya waliosajiliwa na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga Wachezaji waliotumiwa leseni hizo ni Hassani Kessy,Beno Kakaolanya, Andrew Vincent na Juma Mahadhi ambao sasa wanaweza kuitumikia Yanga katika michuano ya ndani na nje.

Ofisa Habari wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania  TFF,  Alfred Lucas amethibitisha kupokea leseni hizo toka CAF na kusema kuwa wachezaji hao wanaweza kuitumikia klabu hiyo katika michuano mbali mbali.

"Ni kweli tumepokea leseni za wachezaji hao toka CAF zinazowawezesha kuitumikia klabu hiyo katika michuano ya ndani na nje" alisema Alfred.
Wachezaji hao walisafiri na kikosi cha Yanga kilichokwenda kuweka kambi nchini Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.

Yanga inaondoka leo Uturuki kuelekea Algeria tayari kwa mtanange huo utakaopigwa siku ya Jumapili.