Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, June 25, 2016

TP MAZEMBE KUTUA KESHO



WAPINZANI wa Yanga, timu ya TP Mazembe inatarajiwa kuwasili kesho na msafara wa watu 32 kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika utakaochezwa Jumanne Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Afisa Habari wa Shirikiso la Soka Tanzania, Alfred Lucas alisema, TP Mazembe wametuma taarifa kuwa watawasili leo na mahali watakapofikia ila muda gani watafika hawajasema.
“TP Mazembe wametuma taarifa kuwa watawasili kesho lakini hawajasema watashuka saa ngapi lakini tunaendelea kuwasiliana nao ili tuweze kuandaa watu wa usalama watakaowapokea kwa sababu TFF ndio wanaratibu kila kitu kwaniaba ya CAF”, alisema Lucas.
TP Mazembe ambao inaongoza kundi A wakiwa na pointi tatu wanakuja kucheza na Yanga ambao hawana pointi baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Mo Bejaia.
Yanga wamerejea jana wakitokea Uturuki baada ya mchezo huo ambapo ilikuwa imeweka kambi awali kwa ajili ya maandalizi ya kuikabili TP Mazembe, mabingwa wa Afrika msimu uliopita.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ukichagizwa na mashabiki wa Simba ambao wanatarajiwa kuishangilia TP Mazembe kulipiza kisasi kwa Yanga baada kuishangilia walipokuja kucheza na Simba miaka mitano iliyopita.


No comments:

Post a Comment