Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, June 17, 2016

STAND UNITED YAISHTAKI TFF FIFA



SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF)  linatuhumiwa na klabu ya Stand United ya  Shinyanga kwamba haiungi mkono uongozi  wa timu hiyo badala yake inafanya kazi na watu wengine ambao wanajiita viongozi baada ya timu kupaa udhamini kutoka ACACIA
Akizungumza jijini, Mshauri wa  ufundi wa Stand United Dkt. Jonas Tiboroha amesema, ushahidi  upo kati ya maafisa wa TFF na baadhi ya viongozi wa kundi ambalo haliungwi mkono na Stand United na hivyo  klabu wameamua kupeleka ushahidi huo FIFA  ili kuona haki yao inapatikana.
“Sisi tumechukua nyaraka  zote ambazo zinahusisha mgogoro huu jinsi abavyo ulikuwa na jinsi ambavyo tunautafsiri kisheria na vielelezo zaidi ya 42 ambavyo tunavipeleka FIFA na tumepeleka kesi saba zinazoonesha namna Stand United inavyo nyang’anywa haki zake mkononi na kundi la watu fulani,” alisema Dkt. Tiboroha
“Wakati sisi tunafanya juhudi kufanya uchaguzi, kumbe kuna mawasiliano upande kwa pili nao wameambiwa pia wafanye uchaguzi, sasa mwisho wa siku TFF watatambua katika uchaguzi upi?”
Stand United imekuwa kwenye mvutano kwa muda mrefu mara baada ya kupata udhamini kutoka kwa kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA.
Baada ya timu hiyo ya Shinyanga kupata udhamini mnono, zilianza kutengenezwa kamati mbalimbali kwa ajili ya kusimamia fedha hizo huku baadhi ya viongozi wa zamani wa timu hiyo wakiwekwa pembeni ya timu hali ambayo imezua mvutano mkubwa.

No comments:

Post a Comment