Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, June 22, 2016

SERENGETO BOYS KAMILI KUIVAA SHELISHELI JUMAPILI


KOCHA wa Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Bakari Shime, amejigamba kuondoka na pointi tatu kwenye mchezo wao dhidi ya Shelisheli utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Jumapili hii.
Akizungumza na gazeti hili Shime alisema timu yake ameiandaa vyakutosha kwani imepata mechi za kimataifa za kirafiki hali iliyomwezesha kukisuka vema kikosi hicho.
“Naamini kwa maandalizi haya tutasonga mbele kwenye hatua inayofuata na vijana wana ari ya kwenda Madgascar 2017 kwenye fainali za mashindano haya”, alisema Shime.
Mchezo huo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 utachezeshwa na waamuzi toka Ethiopia ambao ni Belay Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati na wasaidizi wake ni Tigle Belachew na Kinfe Yilma Kinfe huku mwamuzi wa akiba akiwa  ni Lemma Nigussie na Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys iliingia kambini  Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa Jumapili na marudiano ni Shelisheli  Julai 2, 2016, endapo itafuzu hatua hii itakutana na timu ya Vijana ya Afrika Kusini.
Naye nahodha wa timu hiyo, Issa Makamba amesema wapo tayari kupambana na anaamini ushindi ni wao huku akiwataka mashabiki kuja kuwashangilia.