Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, June 21, 2016

NWITA KUFUNGUA MASHINDANO YA MEYA YA NGUMI ZA RIDHAAMEJA wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, leo anatarajiwa kufungua mashindano ya ngumi za ridhaa ya mkoa wa Dar es Salaam maarufu kama Meya Cup.
Mashindano hayo ambayo yanashirikisha timu toka kwenye taasisi za ulinzi na usalama, wilaya za mkoa wa Dar es Salaam na timu mwaliko toka nje ya nchi yameanza jana kwa mabondia kupima afya na uzito na yatafika tamati Juni 25.
Akizungumza na mtandao huu, Mwenyekiti wa Chama Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es Salaam, Akaroly Godfrey alisema maandalizi yote yamekamilika na timu mwaliko zimewasili.
"Maandalizi yamekamilika na kesho (leo) Mstahiki meya wa jiji, Mwita  ambaye mashindano yanabeba cheo chake atakuwa mgeni rasmi na atatungulia mashindano saa tisa alasiri", alisema Akaroly.
Pia Akaroly alisema timu zinazoshiriki ni Ilala, Kinondoni, Temeke, Ngome, JKT, Polisi Baracks, Mombasa na Nairobi kaunti na timu ya jeshi la Maji toka Nigeria.
Wakati wa zoezi la kupima uzito mabondia walikuwa wakitambiana huku kila mmoja akijigamba kuchukua kombe hilo jambo ambalo linaonesha mashindano ya mwaka huu yatakuwa na msisimko.