Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, June 14, 2016

MICHAEL CARRICK AONGEZA MKATABA MAN UNITED, MOURINHOAMMIMINIA SIFA

English midfielder Michael Carrick has signed a one-year contract extension with Manchester UnitedManchester United imetangaza rasmi kuwa Kiungo wao Mkongwe Michael Carrick amesaini Mkataba wa kumbakisha kwa Mwaka mmoja zaidi hadi Juni 2017.
Carrick, mwenye Miaka 34, alisaini kuichezea Man United kwa mara ya kwanza Julai 2006 na tangu wakati huo amemudu kuisaidia Klabu kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 5, FA CUP, Kombe la Ligi, Kombe la Klabu Bingwa na Ubingwa wa UEFA CHAMPIONS LIGI.

Akiongea mara baada ya kusaini Mkataba mpya baada ya ule wa awali kumalizika, Carrick alisema: “Hii Klabu kubwa kabisa imekuwa sehemu ya maisha yangu kwa Miaka 10, na hivyo nina furaha sana hii safari ya ajabu inaendelea. Ni jambo kubwa sana kupata fursa hii kufanya kazi chini ya Jose Mourinho ambae ana mafanikio makubwa. Napenda kuwashukuru Mashabiki kwa sapoti yao isiyoyumba. Kutwaa FA CUP ilikuwa ni wakati spesho na, tunatarajia, tutatwaa Mataji mengi baadae.”
Nae Meneja mpya wa Man United, Jose Mourinho, alizungumza kuhusu Carrick kubaki: “Michael ni Kiungo mwenye akili sana na msomaji mzuri wa gemu. Nimefurahi sana ameongeza Mkataba. Fomu yake Mwaka huu inaonyesha uwezo wake na furaha yake mchezoni bado iko juu kabisa. Michael ana utajiri mkubwa wa uzoefu kwa kukaa kwake Klabuni hapa Miaka mingi na uzoefu wake utanisaidia sana. Ninangoja kwa hamu kubwa kufanya nae kazi.”
Hiii ni habari nyingine njema kwa Mashabiki wa Man United ambao Jana walipokea kwa shangwe pale ilipoyangazwa kuwa Mourinho amesaini Mchezaji wake wa kwanza baada kumsaini Eric Bertrand Bailly ambae aliekamilisha Uhamisho wake kutoka Villarreal CF ya Spain.