Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, June 24, 2016

JAMIE VARDY, GRIEZMANN WAONGEZA MIKATABA ARSENAL

 

Straika wa England anaechezea Klabu Bingwa ya England Leicester City, Jamie Vardy, ambae amekuwa akitakiwa na Arsenal atabakia Klabuni kwake.
Mapema Mwezi huu, Arsenal iliivamia Leicester na kutoa Ofa ya Pauni Milioni 20 ambayo ndiyo imo kwenye Mkataba wa Vardy akitakiwa na Klabu nyingine na kila dalili zilikuwepo kwamba atahamia Emirates.
Lakini Vardy mwenyewe akasita kutoa uamuzi wa haraka na Wiki iliyopita Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, akanyoosha Mikono juu na kuungama kuwa Straika huyo aliefunga Bao 24 na kuipa Ubingwa Leicester atabakia Leicester.

Leo Leo Leicester imetoa taarifa rasmi kuthibitisha kuwa Vardy, ambae yupo France na Kikosi cha England kinachocheza EURO 2016, atabaki King Power Stadium kuisaidia Timu yake kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa mara ya kwanza Msimu ujao.

Taarifa hiyo imesema wametoa pande zote mbili zinaafiki tangazo lao ili kuondoa utata kuhusu hatima ya Vardy.
Nae Straika wa France Antoine amesaini Dili mpya na Atletico Madrid ambayo itamweka hadi 2021.
Griezmann amekuwa akitangazwa sana kuhamia Klabu za Ligi Kuu England huku mwenyewe akikiri ana furaha kubakia Spain ambako amemaliza Misimu yake Miwili na Atletico akiwa ndie Mfungaji Bora wao.

Magoli ya Griezmann yameisaidia Atletico kumaliza La Liga mara mbili wakiwa Washindi wa Tatu na pia alipiga Bao 7 kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI ambako walitinga Fainali na kutolewa na Real Madrid kwa Mikwaju ya Penati Tano Tano.