Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, June 14, 2016

BLATTER ASEMA KUNA MCHEZO MCHAFU UPANGAJI MASHINDANO YA ULAYABlattter
Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Sepp Blatter amefunguka kuhusu upangaji wa mashindano ya Ulaya na kueleza kuwa kuna mchezo ambao umekuwa ukifanyika wakati wa upangaji wa michezo hiyo.
Akifanya mahojiano na kituo cha La Nacion, Blatter ameeleza kumekuwepo na upangaji wa michezo kwa kutumia mipira ambayo inakuwa ndani ya kapu la kuchanganyia mipira na wanachokifanya ni anayekwenda kuchagua mpira anatumia mpira ambao unakuwa na joto au unakuwa na kawaida.
“Ndiyo, nimeona kwa macho yangu ni kama usaliti … ni katika mashindano ya Ulaya. Unaweza kuona inatumika mipira kwa kuwa ya moto au ya baridi. Nina ushahidi wa hilo.
 UEFA Pot
“Sijawahi kuchota sana mipira, marais wengine walifanya zaidi kwa kuchukua wao wenyewe mipira kutoka katika kikapu,” alisema Blatter.