Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 17, 2016

VAN GAAL UWANJANI LEO OLD TRAFFORD, MANCHESTER UNITED v BOURNEMOUTH USIKU SAA 4.

MANCHESTER UNITED Leo wapo kwao Old Trafford kucheza Mechi yao ya kiporo cha mwisho kabisa cha BPL Ligi Kuu England na Bournemouth iliyoahirishwa Juzi kutokana na sababu za kiusalam
Juzi Jumapili, ndani ya Old Trafford, ambako Man United walitaka ushindi na kuomba City iteleze ili wao watwae Nafasi ya 4 ili wacheze UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI walijikuta wako njia panda baada ya Mechi yao hiyo na Bournemouth kufutwa kabla haijaanza baada ya kugundulika kifurushi chenye kutia shaka kwenye Jukwaa la Stratford End na kulazimisha Watazamaji waondolewe.
Baadae Polisi, wakishirikiana na Kikosi maalum cha Jeshi, kilikilipua Kifurushi hicho na kuendelea kuuchunguza Uwanja mzima.
Baadae, kwa ushauri wa Polisi, Mechi hiyo ikaamuliwa iahirishwe.
Hata hivyo ndoto ya Man United kucheza UCL huenda isitimie kwani wanapaswa Leo kuifunga Bournemouth 19-0 ili kuipikua City Nafasi ya 4 baada ya City Jumapili kutoka 1-1 na Swansea City huko Liberty Stadium.
Kwenye Mechi hiyo City walitangulia kufunga Dakika ya 5 kwa Bao la Kelechi Iheanacho na Swansea kurudisha Dakika ya 46 kwa Bao la Andre Ayew.
Bournemouth wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa hawagombei lolote mbali ya kupanda Nafasi za Msimamo wa Ligi ili kujiongezea Dau la Zawadi za Fedha Timu huambua mwishoni mwa Ligi kuambatani na Nafasi waliyomaliza kwenye Ligi.
Kwa Man United, mbali ya miujiza ya kushinda 19-0 ili kuipiku City kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI wao watabaki kucheza UEFA EUROPA LIGI tu wakibakia Nafasi ya 6 ya BPL walipo sasa au wakitoka Sare au kuishinda Bournemouth na kushika Nafasi ya 5 ambayo pia ni nafasi ya EUROPA LIGI.
Jumamosi Man United pia wana nafasi nyingine ya kucheza EUROPA LIGI ikiwa wataifunga Crystal Palace na kutwaa FA CUP.