Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, May 1, 2016

REAL BETIS 0 v 2 BARCELONA, RAKITIC NA SUAREZ WAIRUDISHA KILELENI BARCA!

Ivan Rakitic dakika ya 50akishangilia bao lake baada ya kufunga bao hilo. Bao la Pili limefungwa na Suarez dakika ya 81 na kufanya Barca kurudi kileleni tena.Barca wanaongoza bao 1-0 mpaka sasa kipindi cha pili, Bao limefungwa na Ivan Rakitic dakika ya 50'
Barcelona waliwachapa Mtu 10 Real Betis 2-0 huku Timu zinazoikimbiza kileleni Atletico Madrid na Real Madrid zikishinda 1-0 kila mmoja.
Bao za Barca hiyo Jana zilifungwa na Ivan Rakitic na Luis Suarez katika Dakika za 50 na 81 dhidi ya Real Betis iliyobaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 35 baada ya Heiko Westermann kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi za Njano 2.
Nao Atletico walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Rayo Vallecano kwa Bao la Antoine Griezman huku Real, wakicheza Ugenini, wakiitungua Real Sociedad 1-0 kwa Bao la Gareth Bale.
Hiyo Jana Real ilicheza bila ya Mastraika wao Cristiano Ronaldo na Karim Benzema ambao ni Majeruhi. Huku zikibaki Mechi 2 Barca wapo kileleni wakiwa na Pointi 85 sawa na Atletico lakini wao wako juu kwa ubora wa Magoli. Real wapo Pointi 1 nyuma yao.

No comments:

Post a Comment