Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 3, 2016

MAROUANE FELLAINI NA ROBERT HUTH KUFUNGULIWA MASHITAKA NA FA

Marouane Fellaini wa United na Beki wa Leicester Robert Huth watajijua Jumanne kama FA, Chama cha Soka England, kitaamua kuwafungulia Mashitaka kwa kuvaana wakati hawana Mpira. 
Tukio hilo lilitokea Jumapili wakati Timu zao zilipopambana kwenye Mechi ya BPL, Ligi Kuu England iliyoisha kwa Sare ya 1-1.
Kwenye tukio hilo, Huth alimvuta Nywele Fellaini na Kiungo huyo wa Man United kulipiza hapo hapo kwa kumpiga na kiwiko na vitendo hivyo havikuonwa na Refa Michael Oliver.
Ikiwa watafunguliwa Mashitaka ya Uchezaji wa Fujo, Wachezaji hao wapo hatarini kupata Kifungo cha Mechi 3 kila mmoja na hili litamaanisha Msimu wao wa Ligi ndio umekwisha. Lakini kwa sababu Man United wamebakiza Mechi 3 za Ligi na Leicester 2 tu, Fellaini anaweza kucheza tena Msimu huu kwenye Fainali ya FA CUP hapo Mei 21 dhidi ya Crystal Palace.