Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 3, 2016

KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU YA TFF YAKAZIA HUKUMU YA KAMATI YA NIDHAMU DHIDI YA TUHUMA ZA KUPANGA MATOKEO LIGI DARAJA LA KWANZA
KIPA Denis Richard Dioniz wa Geita Gold ameshinda rufaa yake aliyowasilisha Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) huku rufaa zingine saba zikitupiliwa mbali.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya rufaa ya nidhamu Wakili Revocutus Kuhuli alisema  kamati yake ilipokea rufani nane za viongozi, mchezaji na timu tatu zilizoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara 2015/2016 lakini kipa Denis pekee aliyeshinda
Uamuzi huo wa Kamati umetangazwa uamuzi huo mbele ya wandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi za TFF, zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Jumla ya rufaa nane zinazohusu timu, kocha, viongozi na mchezaji mmoja zilijadilikuwa na kamati hiyo Mei mosi, 2016 kwenye ofisi za TFF jijini.
Rufaa zilizojadiliwa kwenye kikao hicho ni za Timu ya Geita Gold, Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC, Denis Richard Dioniz - Kipa wa Geita Gold, Fatel Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora
Wengine Salehe Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma, Timu ya Soka ya Polisi Tabora, JKT Oljoro Fc ya Arusha na Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora
Wadau hao wa soka walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu baada ya kamati hiyo kuwatia hatiani na kuwaadhibu kwa makosa ya kupanga matokeo ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza.
Pia Wakili Revocutus alisema kama warufani hawataridhika na hukumu hiyo wanaweza kukataa rufaa ndani ya siku kumi.