Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 3, 2016

JAMIE VARDY NDIE MCHEZAJI BORA WA 2016 KWA WANAHABARI


STRAIKA wa Leicester Jamie Vardy amechaguliwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa 2016 kwa England na FWA, Football Writers' Association, Chama cha Wanahabri wa Soka.
Kufuatia Kura za Wanahabari 290, Asilimia 36 ilimpa Vardy na kuwabwaga wenzake wa Leicester, Riyad Mahrez na N'Golo Kante, waliokuwa wakichuana nae.
Vardy, mwenye Miaka 29, amefunga Bao 29 Msimu huu kwa Klabu yake na England na kuiongoza Leicester kuchungulia Ubingwa wa BPL, Ligi Kuu England.
Mbali ya Vardy, Mahrez na Kante, Wachezaji wengine wa Leicester waliokuwemo kwenye kinyang’anyiro cha Kura za FWA ni Danny Drinkwater, Kasper Schmeichel, Wes Morgan na Danny Simpson
.
Wachezaji wengine waliokuwemo kwenye mchakato wa Kura za Tuzo hii ni Straika wa Tottenham Harry Kane, Kiungo wa West Ham Dimitri Payet, Wachezaji Wawili wa Manchester City Sergio Aguero na Kevin De Bruyne as well as Spurs midfieldepa,oja na Kiungo wa Spurs Dele Alli.
Vardy atatunukiwa Tuzo yake hapo Mei 12 kwenye Hafla maalum Jijini London.
Tuzo hii ya FWA imekuwa ikitolewa kila Mwaka kuanzia 1948/

No comments:

Post a Comment