Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, March 15, 2016

TFF YAREKEBISHA TENA RATIBA LIGI KUU
Machi 16, 2016
Azam FC Vs Stand United
Machi 18, 2016
Kagera Sugar Vs Mtibwa Sugar
Machi 19, 2016
Coastal Union Vs Simba SC
Majimaji Vs Mbeya City
Stand United Vs Ndanda FC
Machi 20, 2016
African Sports Vs Prisons
Machi 21, 2016
Mgambo JKT Vs Toto Africans
Machi 24, 2016
African Sports Vs Toto Africans
Aprili 2, 2016
Majimaji Vs Simba SC
Yanga SC Vs Kagera Sugar
Toto Africans Vs Azam FC
Stand United Vs Mgambo JKT
Ndanda FC Vs Prisons
Mbeya City Vs Coastal Union
Aprili 3, 2016
JKT Ruvu Vs African Sports
Mwadui FC Vs Mtibwa Sugar
Aprili 5, 2016
Toto Africans Vs Yanga SC
Azam FC Vs Ndanda FC
Aprili 9, 2016
Stand United Vs Yanga SC
Ndanda FC Vs Mwadui FC


MECHI mbili za Ligi Kuu Tanzania Bara, za Azam na Yanga zilizopangwa kufanyika mapema wiki ijayo, zimeahirishwa kupisha ratiba ya timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ katika mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.

Mechi hizo ni kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC iliyokuwa ichezwe Machi 22, kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro na Yanga dhidi ya Mwadui FC, Machi 23, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwaka huu.

Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Baraka Kizuguto alisema Taifa Stars itakuwa na mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Chad mjini N’jamena Machi 25 na zitarudiana Machi 28, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Kutokana na ratiba ilivyo baada ya mechi za mwishoni mwa wiki za michuano ya klabu bingwa barani Afrika wachezaji wa Stars wanatarajiwa kukusanyika Jumapili kabla ya safari Jumanne kuelekea Chad,” alisema Kizuguto

Yanga  watarudiana na timu ya APR ya Rwanda Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga walishinda  mabao 2-1.

Na Azam FC watarudiana na Bidvest Wits, Jumapili, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam baada ya kucheza nao na kushinda 3-0 Johannesburg, Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza Kombe la Shirikisho Afrika.
.