Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 10, 2016

SIMBA TENA HAOOOOOO KILELENI





SIMBA, imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara baada ya kuifunga Ndanda FC ya Mtwara kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Imerejea kileleni baada ya Jumanne wiki hii kuenguliwa na bingwa mtetezi Yanga aliyeipiga African Sports kwa mabao 5-0 na kufikisha pointi 50, ilihali Simba ikifuatia kwa kuwa na pointi 48. Lakini ushindi wa jana umeipaisha tena Simba na kufikisha pointi 51 na mabao 40. Yanga ina mabao 51 wakati timu inayoshika nafasi ya tatu ni Azam FC yenye pointi 47, lakini ikiwa imecheza mechi mbili pungufu. Simba imecheza mechi 22 wakati Yanga imecheza mechi 21. Katika mchezo wa jana, Simba ilipata bao la kwanza katika dakika ya 36, mfungaji akiwa Mwinyi Kazimoto aliyeunganisha kwa shuti kali wavuni krosi ya Hassani Kessy. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko. Mabao mengine ya Simba yalipatikana katika kipindi cha pili, mfungaji akiwa raia wa Uganda aliyeichezea Yanga hadi msimu uliopita, Hamisi Kiiza. Alifunga bao la pili katika dakika ya 57 kwa kichwa, baada ya kuifuata kiufundi mpira wa kona uliopigwa na Ibrahim Ajibu ambaye dakika 11 baadaye alipumzishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Danny Lyanga. Bao la tatu kwa Simba lilifungwa katika dakika ya 72, baada ya Kiiza kuinasa pasi ya Lyanga na kuupachika mpira kimiani. Kabla ya mpira kumfikia Lyanga na kutoa pasi, kiungo Justice Majabvi aliachia shuti kali lililotemwa na kipa wa Ndanda mna mpira kumfikia Lyanga. Hata hivyo, ushindi huo haukuwa mwepesi kwa Simba, kwani Ndanda iliyokuwa na nyota kama Atupele Green, Kigi Makasi, Omega Seme, Salvatory Ntebe na wengine, licha ya kufungwa walionesha kandanda safi. Matokeo hayo yanaiacha Ndanda katika nafasi yake ya nane, ikiwa na pointi 24 ilizovuna katika michezo 21. Kikosi cha Simba: Vicent Angban, Hassan ramadhani, Mohamed Hussein, Novaty Lufungo, Juuko Murshid, Justine Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonaes Mkude, Hamisi Kiiza, Ibrahim Ajib na Said Ndemla. Ndanda Kuchele: Jeremias Kisubi, Azizi Sibo, Paulo Ngalema, Kassian Ponela, Salvatory Ntebe, Hemed Khoja, William Lucian, Omega seme, Omary Mponda, Atupele Green na Kigi Makasi.

No comments:

Post a Comment