Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, March 26, 2016

SERENGETI BOYS YAJIANDAA KUIKABILI SHELISHELI







KOCHA Msaidizi wa timu ya Taifa ya Vijana U-17, Bakari Shime amesema wamejipanga vyema katika harakati za kuwania kufuzu fainalia za mataifa ya Afrika kwa vijana yanayotarajiwa kufanyika nchini Madagasca.

Akizungumza na gazeti hili baada ya mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Shime amasema wanaendelea na mazoezi katika uwanja wa Karume kwa wiki mbili kujiandaa na mchezo wa kwanza dhidi ya timu ya Shelisheli.
“Mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya Madagascar tutacheza na Shelisheli hivyo tunajiandaa vyema kuhakikisha tunafanya vizuri,” alisema Shime

Naye nahodha wa timu hiyo, Issa Hajji amesema kila mchezaji anapambana kuhakikisha anabaki ndani ya timu hiyo kutokana na mchujo unaoendelea hivyo ushindani ni mkubwa,” alisema Hajji.

Kwa sasa wachezaji waliopo kambini ni 43 na watafanyiwa mchejo kubakiza 25 ambao wataiwakilisha nchini katika kusaka kufuzu fainali za mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Madagascar 2017.

No comments:

Post a Comment