Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 25, 2016

LEICESTER CITY KUUMANA NA BARCELONA

Klabu ya Leicester City ya Uingereza itacheza dhidi ya miamba wa Ulaya, klabu ya Barcelona kutoka Uhispania, Agosti mwaka huu.
Klabu hizo zitakutana katika dimba la Kombe la Mabingwa wa Kimataifa ambalo huchezwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Viongozi hao wa Ligi ya Uingereza pia watakutana na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain.
Leicester watakutana na Celtic mjini Glasgow tarehe 23 Julai, PSG mjini Los Angeles tarehe 30 Julai na Barcelona mjini Stockholm tarehe 3 Agosti.

Barcelona ndio mabingwa watetezi wa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya.
Klabu hiyo ni miongoni mwa klabu tano za Ligi ya Uingereza zitakazoshiriki michuano hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa huchezewa Marekani.
Klabu nyingine kutoka Uingereza ni Manchester United, Liverpool, Manchester City na Tottenham Hotspur.
Msimu mpya wa Ligi ya Premia utaanza Jumamosi tarehe 13 Agosti.


Ratiba ya Mechi za Klabu Bingwa Kimataifa
  • 23 Julai - Celtic v Leicester, Glasgow
  • 24 Julai - Inter v PSG, Eugene
  • 27 Julai - Real Madrid v PSG, Columbus
  • 27 Julai - Bayern Munich v AC Milan, Chicago
  • 27 Julai - Chelsea v Liverpool, Pasadena
  • 30 Julai - Celtic v Barcelona, Dublin
  • 30 Julai - Inter v Bayern Munich, Charlotte
  • 30 Julai - AC Milan v Liverpool, Santa Clara
  • 30 Julai - PSG v Leicester, LA
  • 3 Agosti - Barcelona v Leicester, Stockholm
  • 3 Agosti - Bayern Munich v Real Madrid, East Rutherford
  • 3 Agosti - AC Milan v Chelsea, Minnapolis
  • (Kuthibitishwa baadaye) - Liverpool v Barcelona
  • (Kuthibitishwa baadaye) - Inter v Celtic
  • (Kuthibitishwa baadaye) - Real Madrid v Chelsea

No comments:

Post a Comment