Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 25, 2016

ADAM JOHNSON AFUNGWA JELA MIAKA SITA

Mchezaji soka Adam Johnson amefungwa jela miaka sita kwa kushiriki mapenzi na msichana wa miaka 15.
Jaji Jonathan Rose amesema mchezaji huyo alitumia vibaya nafasi yake na kumsababishia mwathiriwa wake “madhara makubwa ya kisaikolojia”.
Jaji amemwambia Johnson, 28, kwamba alishiriki ngono na msichana huyo akifahamu vyema kwamba alikuwa na umri wa chini ya miaka 16.

Imebainika pia kwamba polisi walipata kanda chafu za video zinazohusisha wanyama kwenye kompyuta mpakato ya Johnson.
Mahakama ya Bradford iliambiwa kwamba mchezaji huyo alishiriki mapenzi na msichana huyo katika gari lake aina ya Range Rover Januari 2015.
Johnson alichezea timu ya taifa ya England mara 12. Alikuwa mchezaji wa klabu ya Sunderland.

No comments:

Post a Comment