Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, February 20, 2016

MWAMUZI APIGWA RISASI NA MCHEZAJI NA KUFA

 
Refarii mmoja nchini Argentina amepigwa risasi na kuuawa na mchezaji aliyemuonesha kadi nyekundu uwanjani katika mechi ya daraja la pili.

Refarii huyo Cesar Flores alikuwa akisimamia mechi baina ya timu zinazoshiriki ligi ya daraja la chini mjini Cordoba, takriban kilomita 700 Kaskazini mwa Buenos Aires.

Polisi wameanzisha msako mkali kumtafuta mchezaji huyo ambaye hadi sasa hajatajwa.
Refarii Flores alimuonesha kadi nyekundu mchezaji huyo na akaondoka uwanjani kama ilivyo ada.
Lakini baada ya kipindi fulani alirejea akiwa amefoka uwanjani na kumfyatulia refarii huyo risasi 3 ; Kifuani, shingoni na kichwani.

Refarii huyo mwenye umri wa miaka 48 alifariki papo hapo.
Mchezaji mwenza aliyejaribu kumshawishi asimuue refarii alipata majeraha mabaya.
Hii si mara ya kwanza kwa refarii kusini mwa Marekani kushambuliwa kutokana na uamuzi wake uwanjani.
Mwaka uliopita refarii mmoja huko Brazil alilazimika kutoa bunduki ili kumzuia mchezaji mmoja asimshambulie.

No comments:

Post a Comment