Chama cha riadha kwa walemavu Tanzania (Tanzania Paralympic Committee [TPC]) kimepanga kushiriki katika mbio za Kilimanjaro Marathoni zinazodhaminiwa na kampuni ya GAPCO Tanzania wikiendi hii.
Akiongea Dar Es Salaam, Bw. Peter Sarungi, ambaye ni Katibu Mkuu wa TPC, akitoa shukrani zake kwa GAPCO, kampuni inayoongoza katika uuzaji wa mafuta Tanzania kwa kudhamini mashindano ya Mbio za Kilimanjaro Marathoni za KM10 kwa ajili  kwa walemavu, zitawapa wanariadha walemavu nafasi si tu nafasi ya kushindana miongoni mwao lakini pia kutangamana na wanariadha kutoka sehemu mbalimbali duniani. “Tunaamini kwamba hii ni nafasi muhimu kwa TPC ili kutambua wanariadha walemavu ambao wanaweza kuwakilisha Tanzania kimataifa katika matukio mbalimbali ya kimichezo. 
Alieleza kwamba mashindano ya mbio za Kilimanjaro marathon za 10KM kwa walemavu  ambazo zinadhaminiwa na GAPCO ni shindano linalojumuisha baiskeli za walemavu zenye matairi matatu zenye viwango vya kimataifa. Shinando litafanyika tarehe 28 Februari 2016 sambamba na mbio za Kilimanjaro Marathon Moshi, Kilimanjaro na usajili utaanza tarehe 26 Februari 2016. “Mbio hizi ni kwa ajili ya walemavu wote wa Kitanzania, ambapo 60 kati yao watakuwa wakidhaminiwa na GAPCO kushiriki kutoka Dar Es Salaam, Arusha, Moshi na Zanzibar” aliongeza.
Tangu GAPCO ilipoanza kudhamini Marathon mwaka 2011, wameshuhudia maendeleo chanya mwaka hadi mwaka katika ubora wa mashindano. “ Tunashukurum jitihada za GAPCO, si tu katika kufanikisha shindano hili kupitia udhamini wake lakini zaidi ni  kutoa msaada wa mahitaji maalumu kwa washiriki wenye ulemavu katika mfumo wa chakula na usafiri.” alisema MrSarungi. “Pia tunafuraha kuhusu kuongezeka kwa zawadi ya fedha taslimu kwa mshindi ambapo ni Tsh. 1,000,000 kiasi hiki kinaweza kubadili maisha ya washindi.
Bw. Sarungi amewasihi watanzania kujitokeza kwa wingi kuwashangilia wanariadha watakaoshiriki mbio hizi. “Tunataraji kushiriki na tunachukua nafasi hii kuwakaribisha Watanzania kujitokeza na kuwapashangilia wanariadha wetu katika tukio hili”.
Chama cha riadha kwa walemavu Tanzania (Tanzania Paralympic Committee [TPC]) ni chama cha kitaifa na kimataifa kinachotambulika na Serikali kupitia Baraza la Sanaa Tanzania na Chama cha ridhaa kwa walemavu cha Kimataifa (International Paralympics Committee [IPC]). TPC imekusudia kuwaleta pamoja wanariadha walemavu kutoka Tanzania kupitia matawi ya kimikoa na kiwilaya na makundi mengine yenye hulka zinazoshabihiana (shule za walemavu na timu za michezo).