Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, February 22, 2016

DROO, RATIBA YA COPA AMERICA CENTENARIO 2016, TAYARI, KUANZA JUNI HUKO USA

MICHUANO YA MATAIFA YA Marekani ya Kusini safari hii itanyika huko USA yakiwa ni Mashindano maalum ya kusheherekea Miaka 100 na kujumuisha Nchi 16 zikiwemo Nchi waalikwa wakiwemo Wenyeji USA na Jana Droo ya kupanga Makundi.
Makundi Manne yenye Timu 4 kila moja yamepangwa na Mabingwa Watetezi Chile wapo Kundi D pamoja na Argentina, Panama na Bolivia.
Michuano hii itachezwa kwenye Viwanja 10 vinavyopakia Washabiki zaidi ya 50,000 kila kimoja ambavyo ni Santa Clara, Seattle, Pasadena, Glendale, Houston, Chicago, Philadelphia, East Rutherford, Foxborough na Orlando.
Wenyeji USA, ambao wapo Kundi A, watafungua dimba hapo Juni 3 kwa kucheza na Colombia huko Santa Clara, California. 
Fainali itachezwa Juni 26 ndani ya MetLife Stadium, East Rutherford.
KUNDI A
USA, Colombia, Costa Rica, Paraguay
KUNDI B
Brazil, Ecuador, Haiti, Peru
KUNDI C
Mexico, Uruguay, Jamaica, Venezuela
KUNDI D
Argentina, Chile, Panama, Bolivia