Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 12, 2015

YAYA TOURE AWA MCHEZAJI BORA AFRIKA, AINGIA KWENYE REKODI MPYA

Toure
Kiungo wa klabu ya Manchester City ya England na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure ametwaa tunzo ya mchezaji bora Afrika inayotolewa na Shirika la Utangazaji nchini England (BBC) kwa mwaka 2015.
Toure anaingia kwenye orodha ya wachezaji watatu ambao wamewahi kutwaa tunzo hiyo mara mbili akiungana na Nwanko Kanu pamoja na Jay-Jay Okocha (wote wa Nigeria) ambao waliwahi kutwaa tunzo hiyo mara mbili.
Nyota huo wa Ivory Coast amesema anajivunia kuwa mshindi wa tunzo hiyo ambayo mshindi hupatikana kwa kupigiwa kura na mashabiki.
“Najivunia sana. Kupokea tunzo hii kutoka kwa mashabiki siamini”., Toure ameiambia BBC Sport.
Yaya Toure amewashinda Yacine Brahimi (Algeria), Pierre-Emerick Aubameyang (Gagon), Andre Ayew (Ghana) na Sadio Mane (Senegal) ambao walikuwa wakiwania tunzo hiyo kwa mwaka 2015.