Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 12, 2015

YANGA KUANZA KARATA YAKE FEBRUARI MWAKANI KOMBE LA MABINGWA



MABINGWA wa Tanzania, Yanga  wataanza na Cercle de Joachim ya Mauritius katika raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, wakati Azam FC itaanzia raundi ya kwanza.
Azam FC itakutana na mshindi kati Bidvest Wits ya Afrika Kusini na wawakilishi wa Shelisheli amabo hawajapatikana.
Yanga itaanzia nyumbani kati ya Februari 12, 13 na 14 mwakani huku ikimalizia ugenini kati ya Februari 26, 27 na 28 na ikivuka hatua hiyo, 
itakutana na mshindi kati ya APR ya Rwanda na Mbabane Swallows ya Swaziland.
Ikivuka hatua hiyo, itakutana na Al Ahly ya Misri, au mshindi kati ya Recreativo de Libolo ya Angola na Racing Micomiseng ya Equatorial Guinea.
Azam FC itaanzia kucheza ugenini kati ya Machi 11, 12 na 13 kabla ya kumalizia nyumbani kati ya Machi 18, 19 na 20 na ikivuka mtihani huo, itakutana na ama Esperance ya Tunisia, wawakilishi wa Chad au News Stars de Douala ya Cameroon.
Mabingwa wa Zanzibar, Mafunzo wataanzia Raundi ya awali na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati JKU itacheza na Gaborone ya Botswana katika Kombe la Shirikisho.

No comments:

Post a Comment