Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 12, 2015

MAJWEGA, KIONGERA, KUCHEKI MECHI WAKIWA JUKWAANI LEO

Kiungo wa Simba aliyesajiliwa kutoka Azam FC Brian Majwega
Kiungo wa Simba aliyesajiliwa kutoka Azam FC, Brian Majwega
Wakati klabu ya Simba ikiwa imefanya usajili katika kipindi cha dirisha dogo kuhakikisha inakiongezea nguvu kikosi chake, taarifa zinadai kwamba, wachezaji hao waliosajiliwa katika kipindi cha dirisha dogo hawataruhusiwa kucheza kwenye mchezo dhidi ya Azam FC utakaochezwaa leo kwenye Uwanja wa Taifa .
Wachezaji hao hawatacheza kwa sababu bado hawajathibitishwa na kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya TFF ili waanze kuitumikia klabu hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa ina matarajio ya kuwatumia  kuiangamiza Azam.
Mshambuliaji wa Simba Paul Kiongera
Mshambuliaji wa Simba Paul Kiongera
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi,  Boniface Wambura, amesema kamati ya sheria na hadhi za wachezaji hukutana mara baada ya dirisha la usajili kufungwa kwa ajili ya kuidhinisha usajili wa wachezaji wa Klabu ikiwa ni pamoja na kupitia pingamizi zilizowekwa kwa wachezaji mbalimbali.
“Kanuni za usajili au kanuni za ligi zinasema klabu au timu inamwombea usajili mchezaji kwa TFF kwani ndiyo inaidhinisha usajili baada ya TFF kuidhinisha ndipo mchezaji anapata liseni au mchezaji anaweza akawa ameidhinishwa lakini hata hati ya uhamisho wa kimataifa lakini itakapofika tu acheze”, amesema Wambura.
“Lakini mpaka sasa hivi kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ambayo ndiyo inathibitisha usajili haijakutana kwahiyo ikikutana watu wakapata liseni wanaweza wakacheza lakini kama hawajapata liseni ni wazi hawawezi kucheza mpaka kamati itakapokuwa imekaa”.
Lakini kamati mpaka sasa bado haijakutana kwahiyo wachezaji wote waliosajiliwa katika dirisha dogo hawatakuwa na uhalali wa kucheza katika michezo ya ligi kuu Tanzania bara itakayopigwa leo na kesho.
Kwahiyo wachezaji kama Brian Majwega, Paul Kiongera na Dany Lyanga hawatapata nafasi ya kucheza kwani hadi sasa kamati ya sheria na hadhi za wachezaji bado haijakutana kuidhinisha uhalali wa wachezaji wote waliosajiliwa kwenye dirisha dogo na mara nyingi kamati hukuta mara baada ya dirisha la usajili kufungwa.