Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, December 16, 2015

KOZI YA MAKOCHA WA NGAZI YA CHINI (GRASSROOT) YASHIKA KASI KARUME, DAR ES SALAAM

KOZI ya walimu wa mpira wa miguu ngazi ya chini (Grassroots) inayofayika katika ukumbi wa TFF uliopo Karume jijini Dar es salaam imeshika kasi baada ya walimu hao kuanza mazoezi ya vitendo leo.
Kozi hiyo ilifunguliwa jana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine ambapo washiriki 30 wanatakiwa kwenda kuwafundisha na kuupenda mpira wa miguu watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 6-12.
Walimu hao wanatoka katika mikoa ya Dar es salaam, Mtwara, Lindi na Ruvuma wanatakiwa kusaidia katika kukuza mpira wa miguu ambao chimbuko lake ni watoto wadogo kuupenda na kucheza mpira
Kozi hiyo inaendeshwa na mkufunzi wa FIFA kutoka nchini Mauritius, Govinden Thondoo ambaye ametoa pongezi kwa TFF kwa kuwa na maendeleo mazuri katika kozi ya Grassroot kulinganisha na nchi nyingine zilizopo katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati wenye nchi 15.
Jumla ya walimu 106 kutoka katika shule za msingi za mikoa mbalimbali nchini Tanzania zina makocha waliopata kozi za Grassoort katika kipindi cha miaka 2, na lengo likiwa ni kufikisha walimu 25,000.