Mkuu wa
Wilaya ya Kaliua Tabora, Venance Mwamoto (katikati) Kulia ni Mwenyekiti wa DABA, Akaloli Godfrey, na kushoto ni Mkuu wa kambi ya 831KJ, Luteni Kanali, Erasmus Bwegoge |
Wanamichezo wakiwa wamesisima wakati mgeni rasmi akiingia pamoja na mkuu wa kambi |
Wana michezo wakisikiliza kwa makini |
MKUU wa
kambi 831KJ, ya Mgulani, Luteni Kanali, Erasmus Bwegoge amewaahidi wanamichezo
wa kikosi hicho ushirikiano wa hali na mali ili kuendelea kufanya vizuri kwenye
michezo.
Luteni
Kanali Bwegoge aliyasema hayo kwenye hafla ya kukabidhiwa kombe la mashindano
ya meya yaliyoandaliwa na chama cha ngumi za ridhaa, mkoa wa Dar es Salaam
(DABA) ambapo timu ya ngumi ya Mgulani ndio iliibuka bingwa wa jumla.
“Kwanza naombeni mtambue mna mkuu wa kambi
ambaye ni mdau wa michezo kwa kudhihirisha hilo nawaahidi kushirikiana nanyi
katika michezo ili tulete sifa kwenye kambi, mkoa na hatimaye taifa kwa
ujumla”, alisema Luteni Kanali Bwegoge
Awali
akikambidhi kombe hilo, Mkuu wa wilaya ya Kaliua, Tabora, Venance Mwamoto
ambaye pia ni mlezi wa DABA, aliwapongeza wachezaji hao kwa kuweza kutetea
ubingwa wao na kuwataka kuendelea dhamira hiyo ya michezo kwani michezo
inakwenda sambasamba na nidhamu na
jeshini ndipo nidhamu ilipozaliwa na kukulia.
“Wanajeshi
najua wana nidhamu na michezo na nidhamu ni ndugu hivyo nitashirikiana na mkuu
wenu wa kambi na chama cha DABA kuhakikisha mnashiriki mashindano mengi na
ikiwezekana ya kimataifa”, alisema Mwamoto.
Naye
Mwenyekiti wa DABA, Akaloli Godfrey aliipongeza timu ya JKT Mgulani kwa kuweza kuibuka bingwa kwa
mara ya pili mfufulizo na kuwaahidi endapo wataweza kulitetea kombe hilo kwa
mara ya tatu basi litakuwa la kwao.
Mashindano
ya Meya yalifanyika Agosti 5-8 kwenye Uwanja wa ndani wa taifa na kushirikisha
timu 13, MM Mgulani akaibuka bingwa wa jumla kwa pointi 19, nafasi ya pili
ikachukuliwa na Ngome ambayo ilipata
pointi 18.
No comments:
Post a Comment